SERIKALI INATHAMINI MCHANGO WA ASASI ZA KIRAIA-MHE. KAPINGA



SERIKALI INATHAMINI MCHANGO WA ASASI ZA KIRAIA-MHE. KAPINGA

Na,Saleh Lujuo-Dodoma

Serikali kupitia wizara ya Nishati imesema  inathamini mchango mkubwa wa Asasi za kiraia Kwenye Masuala ambayo yanahusu maendeleo ya watanzania.

Akizindua jukwaa la Mwaka la uziduaji la Hakirasilimali leo Novemba 9,2023 jijini Dodoma, Naibu waziri wa Nishati Mhe. Judith Kapinga amesema jukwaa la uziduaji ni jukwaa muhimu katika kujadiliana namna gani ya kuwekeza katika vyanzo ambavyo ni rafiki kwa mazingira.

"Sisi kama serikali tutaendelea kuangalia Ni namna gani watanzania wananufaika na matumizi ya rasilimali tulizonazo kwa maendeleo yao binafsi na Taifa kwa ujumla". Amesema 

Aidha, amewapongeza Hakirasilimali kwa kuandaa Jukwaa hilo na kuwaleta wadau mbalimbali ili kubadilishana mawazo namna gani ya kutumia rasilimali kwa maendeleo na namna ya kutunza Mazingira.

"Dunia nzima tunapitia changamoto kubwa ya kimazingira,hivyo tukikutana katika mikutano kama hii na tukabadilishana mawazo inatusaidia sana sisi kama serikali kuweza kuboresha Mipango yetu ili kuweza kuwanufaisha watanzania zaidi kupitia rasilimali ambazo tunazo". Amesema

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Hakirasilimali,Adam Anthony amesema siku mbili watakazokaa watajadili kwa kina sekta ya uziduaji ikiwa ni pamoja na ushiriki wa wazawa katika Mnyororo wa thamani,Mazingira rafiki ya uwekezaji, haki za binadamu,uwazi wa Mikataba na utoaji wa leseni, ushiriki wa wanawake katika sekta, na nafasi ya wachimbaji wadogo katika sekta.

"HakiRasilimali inaamini kuwa uwazi na uwajibikaji katika sekta ya uziduaji ndio chachu ya maendeleo ya sekta na Taifa kwa ujumla". Amesema.

Sambamba na hayo amesema kuwa HakiRasilimali ni Mwamvuli wa Asasi za kiraia 16, zinazofanya Tafiti, uchambuzi wa sera na sheria, na uchechemuzi Kwenye sekta ya uziduaji, Madini,Mafuta na Gesi Asilia nchini Tanzania.

Jukwaa la Uziduaji kwa Mwaka 2023 limebebwa na kaulimbiu isemayo: kufanikisha Mhamo wa Nishati na Maendeleo endelevu katika sekta ya uziduaji Tanzania.

Post a Comment

Previous Post Next Post