MGENI RASMI MBIO ZA KONGWA AFRICAN LIBERATION MARATHON 2023 ANATARAJIWA KUWA DKT. DAMAS NDUMBARO


MGENI RASMI MBIO ZA KONGWA AFRICAN LIBERATION MARATHON 2023 ANATARAJIWA KUWA DKT. DAMAS NDUMBARO

Na,Saleh Lujuo-Dodoma

Serikali ya Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma imeandaa mbio zinazogusia ukombozi Kusini Mwa Afrika zijulikanazo kama Kongwa African Liberation Marathon zenye lengo la kuonyesha thamani ya Tanzania pamoja na Mkoa wa Dodoma na kuonyesha mchango wa wilaya ya Kongwa katika harakati hizo za ukombozi.

Mkuu wa Wilaya hiyo Remidius Mwema akizungumza na waandishi wa habari Novemba 16,2023, Jijini Dodoma amesema mgeni rasmi katika mbio hizo ni Waziri wa Utamaduni,Sanaa na michezo Dokta Damas Ndumbaro na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemarry Senyamule.

"Mbio hizo zimeandaliwa na kwa kushirikiana na wadau mbalimbali  wa maendeleo nchini na zitafanyika Novemba 25,2023,wilayani humo". Amesema

Mwema amesema mbio hizo zitakuwa endelevu kwakufanyika kila mwaka na watazitumia kutangaza fursa mbalimbali ziliopo katika wilaya hiyo.

"Kupitia mbio hizo Wilaya ya Kongwa itaendelea kutoa elimu kwa umma juu ya umuhimu wa kuyatambua maeneo ya kihistoria, kuyalinda, na kuyaendeleza ili kuenzi historia ya Taifa na kuyafanya kuwa sehemu ya utalii wa kihistoria katika maeneo ya urithi wa ukombozi yaliyopo nchini". Amesema

"Niwaombe wana Dodona na mikoa jirani kujitokeza kwa wingi kushiriki kikamilifu kuendelea kutangaza fursa zetu". Ameongeza

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi  yam bio hizo Kelvin Msumule amesema hadi sasa maandalizi yanaendelea vizuri na yamefikia asilimia 98.

"Sisi kama kamati tumejipanga kwa Asilimia 98 hadi Sasa na hizi Asilimia mbili zilizobaki ni zasiku Moja kabla ya mbio kukimbiwa kwa mana ya kwamba ya utekelezaji ya vitu ambavyo vinatutaka vifanyike kwa siku hiyo". Amesema

Mbio hizo zitakuwa za Kilomita 5,10 na 21 ambapo zawadi zitatolewa  kwa washindi wa kwanza,wapili na watatu.

Post a Comment

Previous Post Next Post