TUNATAKA VIJANA WABEBE TAIFA MOYONI MWAO NA SIYO MIDOMONI MWAO-DKT. SAMIA SULUHU HASSAN



TUNATAKA VIJANA WABEBE TAIFA MOYONI MWAO NA SIYO MIDOMONI MWAO-DKT. SAMIA SULUHU HASSAN

Na,Saleh Lujuo-Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan ameielekeza Wizara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa kuandaa mpango mkakati wa kurekebisha makambi kwenye Jeshi la JKT katika upande wa malezi ya vijana pamoja na kuliwezesha Shirika la SUMA JKT kupata mikopo ili wazalishe Kwa kiwango kikubwa na waweze kurejesha mikopo.


Maelekezo hayo yametolewa leo jijini Dodoma na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ambapo amesema dhamira ya Serikali ni kuiboresha JKT ili liwe Jeshi la kisasa zaidi linaloendana na wakati na kutimiza majukumu yake kwa ufanisi wa hali ya juu.

"Dhamira ya Serikali ni kuiboresha JKT ili liwe Jeshi la kisasa zaidi linaloendana na wakati na kutimiza majukumu yake kwa ufanisi wa hali ya juu, mafunzo yanayotolewa na JKT yawasaidie vijana kuwa wazalendo wa kweli wanaothamini utaifa, umoja na mshikamano wa Watanzania na wanaopenda kufanya kazi kwa moyo wa kujituma na kujitolea". Amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Sambamba na hayo Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amewataka vijana watakaoendelea na kazi katika Vyombo vya Ulinzi na Usalama baada ya  mafunzo yao, wanatakiwa wawe na weledi wa kuaminika, kutumainiwa na wanaoweza kuilinda na kuitetea nchi yao bila hofu.

Kwa upande wake waziri wa ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Mhe. Innocent Bashungwa, amesema kuwa Wizara itaendelea kushirikiana na wizara za kisekta kuboresha mafunzo stadi za kazi kwa vijana wa JKT na kuwawezesha kuwapatia ujuzi na maarifa zaidi.

"Kwa vijana watakaoendelea na kazi katika Vyombo vya Ulinzi na Usalama baada ya  mafunzo yao, nataka wawe na weledi wa kuaminika, kutumainiwa na wanaoweza kweli kuilinda na kuitetea nchi yao bila hofu.
Kwa upande wake waziri wa ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa, amesema kuwa Wizara itaendelea kushirikiana na wizara za kisekta kuboresha mafunzo stadi za kazi kwa vijana wa JKT na kuwawezesha kuwapatia ujuzi na maarifa zaidi". Amesisitiza Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Naye Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Jacob John Mkunda ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuzitafutia ufumbuzi changamoto zilizopo kwa kulipatia Jeshi  rasilimali mbalimbali kwa nia ya kuliwezesha kutimiza malengo yake kwa ufanisi.

"JWTZ kwa kushirikiana na Wizara ya Ulinzi na JKT, tumeweka mikakati ya kuliboresha na kulifanya Jeshi la Kujenga Taifa kuwa la kisasa zaidi ili liweze kwenda sambamba na mabadiliko ya sayansi na teknolojia duniani". Amesema Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Mkunda.

Akitoa Taarifa ya Jeshi la kujenga Taifa (JKT),
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, Meja Jenerali Rajabu Nduku Mabele ametaja changamoto ya Miundombinu na upungufu wa makambi ya Majeshi nchini ni sababu Moja wapo inayokwamisha vijana wengi kutochukuliwa kujiunga na jeshi kwa mujibu wa sheria.

"Uanzishwaji wa vikosi, kambi mpya za JKT na ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya vikosi, umesaidia kuongeza idadi ya vijana wanaoshiriki mafunzo ya JKT. JKT imekuwa ni chombo muhimu cha muwajenga vijana na kukuza uzalendo". Amesema Meja Jenerali Mabele.

Kauli mbiu ya kilele Cha madhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la kujenga Taifa (JKT) ni Malezi ya vijana, uzalishaji Mali na Ulinzi Kwa ustawi wa Taifa ambapo Dhima  ya JKT ni kuwalea vijana wa kitanzania, ili kuwajenga kinidhamu,uzalendo, ukakamavu na kuwafundisha ujuzi na hatimaye kuchangia katika ulinzi wa Taifa na maendeleo ya kiuchumi.






Post a Comment

Previous Post Next Post