SERIKALI IMEDHAMIRIA KUDHIBITI MATUMIZI YA FEDHA ZA UMMA KWA KUTUMIA NJIA MBALIMBALI IKIWEMO MIFUMO YA KIELEKTRONIKI.

SERIKALI IMEDHAMIRIA KUDHIBITI MATUMIZI YA FEDHA ZA UMMA KWA KUTUMIA NJIA MBALIMBALI IKIWEMO MIFUMO YA KIELEKTRONIKI.

Na,Saleh Lujuo-Dodoma.

Mamlaka ya udhibiti ununuzi wa umma (PPRA) imesema Mwelekeo wa Serikali kwenye ununuzi wa umma utajikita kwenye matumizi ya teknolojia zaidi kwa kushirikina na wadau wengine pamoja na kuandaa mkakati wa kitaifa wa ununuzi wa umma kwa njia ya mtandao na kutoa kanuni elekezi za mageuzi ya kidijitali kwenye Ununuzi wa Umma.

Kauli hiyo imetolewa leo Julai 17,2023 Jijini Dodoma na Afisa Mtendaji Mkuu wa mamlaka ya udhibiti ununuzi wa umma, Bw, Eliakim Maswi, wakati akieleza utekelezaji wa majukumu ya Taasisi hiyo na Mwelekeo wa utekelezaji Kwa mwaka 2023/2023 ambapo amesema serikali imeendelea kudhibiti matumizi ya fedha za umma kwa kutumia njia mbalimbali ikiwemo mifumo ya kielektroniki ili kuleta tija na ufanisi unaostahili katika utekelezaji wa Bajeti husika.

"Mamlaka imekasimiwa jukumu la kusanifu, kuanzisha na kuhuisha mifumo mbalimbali ya kielektroniki kwa ajili ya kuweka uwazi na kuleta tija kwenye ununuzi wa umma". Amesema Bw.Eliakim

Aidha,Bw. Eliakim ametoa wito kwa wanaojihusisha na ununuzi wa umma ikiwemo watumishi wa umma na wazabuni kuzingatia maadili katika utendaji wao na kufuata taratibu na kanuni zinazoongoza eneo la ununuzi wa umma.

"Mamlaka haitasita kuwachukulia hatua kwa mujibu wa sheria wale wote watakaokiuka taratibu au watajihusisha na uovu wowote utakaoisababishia Serikali hasara". Amesema Eliakim.

Sambamba na hayo Mamlaka imekusudia kufanya maboresho ya Sheria ya Ununuzi wa Umma ili kukidhi mahitaji ya wateja yaliyopo sokoni ikiwa ni pamoja na kuondoa urasimu usiokuwa wa lazima na kuongeza uwajibikaji kwa wale wote wanaojihusisha na ununuzi wa umma.

Mamlaka ya Udhibiti Ununuzi wa Umma (PPRA) imeanzishwa kwa lengo la kuhakikisha upatikanaji wa thamani ya fedha katika ununuzi na ugavi, kuhakikisha uzingatiaji wa haki, ushindani, uwazi, uendelevu, uwajibikaji, matumizi mazuri ya fedha, ufanisi na uadilifu katika ununuzi na ugavi.

Post a Comment

Previous Post Next Post