TUHAMASISHE UTALII WA NDANI TUKUZE PATO LA TAIFA



TUHAMASISHE UTALII WA NDANI TUKUZE PATO LA TAIFA

Na,Saleh Lujuo-Dodoma.

Kampuni ya Mtembezi Marathoni Present imeeanda mbio za Mtembezi Marathon kwa Mkoa wa Dodoma zinazotarajiwa kufanyika July 7 mwaka huu zenye lengo la kuhamasisha wananchi kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii nchini ili kukuza pato la Taifa.

Akizindua jezi ambayo itatumika katika mbio hizo Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini,Jabiri Shekimweri,ametoa wito Kwa wakazi wa Mkoa huo kujitokeza Kwa wingi kushiriki mbio za  mtembezi marathon  ambazo zinatarajiwa kufanyika July 7 mwaka huu.

Shekimweri amesema ofisi yake Kwa kushirikiana na Mtembezi Adventure wamekubaliana kufanya bio hizo zitakazo ambatana na kutangaza utalii wa ndani na kuutangaza Mkoa wa Dodoma.

" Mkoa wa Dodoma una utalii mwingi Kuna utalii wa  Ngoma,utalii wa kilimo Kwa maana ya zabibu na mapori ya akiba, mji wa Serikali Mtumba, Barabara ya mzinguko na vingine vingi vya kiutamaduni ambavyo vinavutia hivyo kufanyika Kwa mbio hizo kutasaidia kutangaza utalii uliopo ndani ya mkoa wetu, niwaalike wananchi wa Mkoa huu kujitokeza Kwa wingi kushiriki mbio hizo"

Akitoa maelezo mafupi kuhusu umuhimu wa vivutio vya utalii,Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa TANAPA, Dkt, Noelia Myonga,Amesema wanatambua thamani ya michezo katika kutangaza utalii hapa nchini ambapo amesema mbio hizo ni vema zikaambatana na kuutangaza utalii wa ndani kwani unachangia kwa kiasi kikubwa kukuza uchumi wa nchi.

"Tunatamani utalii huu uambatane na utalii wa kawaida kwakuwa hapa Dodoma pia tuna mambo mengi ya kitalii, Kuna utalii wa kilimo,utamaduni na chakula  hivyo tuko tayari kushirikiana na wadau mbalimbali kutangaza utalii wa ndani"

Kwa upande wake Mkurugenzi wa mtembezi adventure  present Samson  Samweli, amesema wameandaa  Mtembezi  marathoni mkoa wa Dodoma Kwa kuhamasisha utalii wa ndani wa Mkoa huo pamoja na kuwahamasisha wananchi kufanya mazoezi mara kwa mara ili kuepuka kupata maradhi yasiyo ya kuambukiza.


"Mtu anaweza kuuliza kwanini tumeandaa mbio hizi Dodoma kunautalii gani?, Dodoma kunautalii mwingi sana ,unaotokana na shughuli za kijamii kama kilimo na tamaduni, mapori ya akiba na nyingine nyingi".

Kuhusu zawadi zitakazotolewa , Kwa washindi watatu,Bw Samson amesema zitatolewa na kampuni ya gesi ya Orxy ikiwa ni mbio za kilomita 21,10 na kilomita 5.


Mtembezi Marathon kwa mkoa wa Dodoma 2023 umeambatana na kauli mbiu isemayo "Tuhamasishe utalii wa ndani tukuze pato la Taifa".

Post a Comment

Previous Post Next Post