Na,Saleh Lujuo-Dodoma.
Serikali kupitia Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL),linatarajia kujenga minara 54 kwenye Kata 104 na vijiji ili kuendelea kutoa huduma hiyo kwa Kata 130 ambapo huduma hiyo itaboresha mawasiliano na kuwa kichocheo kiuchumi,kijamii na kiutamaduni.
Akizungumza na wandishi Wa Habari baada ya hafla ya makubaliabo ya kutia saini mikataba ya kupeleka huduma ya mawasiliano vijijini baina ya UCSAF na watoa huduma za mawasiliano Leo Mei 13,2023,Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo Mhandisi Peter Ulanga amesema kuwepo Kwa huduma Bora za mawasiliano,hususan Katika maeneo ya vijinini ni muhimu sana kiuchumi na kijamii.
Amesema katika minara hiyo Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) walishinda zabuni katika kata 104 na watajenga minara 104, Vodacom Tanzania amelishinda kata 190 watajenga minara 190, Airtel Tanzania walishinda kata 161 na watajenga minara 168 , Tigo walishinda zabuni katika kata 244 na watajenga minara 262 na Haloteli walishinda zabuni katika kata 34 na watajenga minara 34.
Katika kuboresha huduma za mawasiliano nchini Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa Shirika limeingia makubaliano na Shirika la Posta kwa ajili ya kutoa huduma za uwakala mkuu wa T-PESA, usambazaji wa vocha na usajili wa wateja wapya wa TTCL.
Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote(UCSAF) Justina Mashiba amesema Mfumo huo ulitangaza zabuni ya kupeleka huduma za mawasiliano katika maeneo 763 na Baada ya mchakato huo walipata maeneo katika kata 713 ambayo minara ya mawasiliano 758 itajengwa.
"Ushiriki wa watoa huduma katika zabuni hii wameweza kushiriki Kwa asilimia 93,hii pia ni historia iliyowekwa katika ushirikiano baina ya serikali na sekta binafsi" Amesema Mashiba.