Na,Saleh Lujuo-Dodoma.
Serikali kupitia Wizara ya Habari Mawasiliano na teknolojia ya Habari,imeridhia kuiongezea muda wa miezi sita Kamati ya Tathmini ya hali ya uchumi kwa Vyombo vya Habari na Wanahabari nchini ili iweze kufanya kazi yake kwa ufanisi zaidi.
Waziri wa Habari,Mawasiliano na teknolojia ya Habari,Nape Nauye ametoa kauli hiyo leo Jijini Dodoma mara baada ya Kukutana na Kamati hiyo ambapo amesema Tasnia ya Habari inachangamoto zake haiwezi kumalizwa na Matamko ya kisiasa bali zitamalizwa kwa kutengeneza Mifumo na Tafiti.
''Tasnia ya Habari inachangamoto zake, haziwezi kumalizwa na matamko ya kisiasa, zitamaliza kwa kutengenza mifumo, mifumo inatengezwa kwa tafiti mifumo inatengenezwa kwa kuhusisha mawazo ya watu wengi ndio maana tumeipa kamati kazi hiyo''amesema waziri Nape.
Katika hatua nyingine Waziri Nape ametoa wito kwa wadaiwa wote ambao wanadaiwa na Vyombo mbalimbali vya Habari hapa nchini kulipa madeni hayo.
''Na kwa sababu haya madeni yako katika Taasisi mbalimbali yapo yale ambayo wanadaiwa Halmashauri kule chini zinadaiwa taasisi za serikali,zinadaiwa Wizara kote kule tutakachofanya baada ya Bajeti kupita na baada ya Tamko lile la Rais na la kwangu bungeni tutaweka utaratibu wa namna haya madeni yatalipwa nataka niwahakikishie kwamba yatalipwa si lazima yalipwe yote mara moja lakini walau ila yanze kulipwa''amesema Waziri Nape.
Awali Mwenyekiti wa Kamati ya kutathmini hali ya uchumi kwa Vyombo vya Habari na wanahabari,Tido Mhando ameiomba Serikali kuwaongezea muda kutokana na kazi hiyo kuhitaji utafiti wa kitaalam zaidi.
Wakati tumejipanga Mhe.Rais nae anatoa kauli ambayo tumeisikia kwamba kama vile tulikuwa nae kwa sabbu kile kile alichokisema yeye ndicho ambacho wataalam walikuwa wametushauri na sisi tumekubaliana na ndio sababu leo tukasema kwa kuwa mlishakuwa na shauku waandishi na wengine kuweza kutaka kujua tunaendeleaje sababu jambo hili linawahusu tukaona ni vizuri tuje mbele yenu tuwaeleze tulichokifanya na sasa tunataka kufanya nini''.amesema Tiddo Mhando.
Kamati hiyo iliundwa rasmi Januari 23 Mwaka huu ikiwa na Wajumbe tisa ikiongozwa na Mwenyekiti wake Tido Mhando na Katibu ni Gerson Msigwa ambapo kamati hiyo inatarajiwa kukamilisha kazi yake mnamo Mwezi Novemba Mwaka huu.