BASHE AZINDUA RASMI USAJILI KWA AJILI YA WASHIRIKI WA KONGAMANO LA USALAMA WA CHAKULA

 

Na,Saleh Lujuo-Dodoma.

Waziri wa kilimo Mh Hussein Bashe Leo Mei 12.2023 amezindua Rasmi usajili Kwa ajili ya washiriki Wa kongamano la usalama Wa chakula litakalo fanyika septemba 4-8 Mwaka huu jijini Dar es salaam.

Akizungumza leo jijini Dodoma waziri Bashe amesema kongamano hilo litaangazia nafasi ya Bara la Africa katika matumizi ya mbinu bunifu zitakazohakikisha dunia inakuwa na usalama Wa chakula.

"Nawaalika wadau Wa kilimo wakiwemo wataalam wa masuala ya Mifumo ya chakula Duniani,nasisitiza pia umuhimu na nafazi ya viongozi wa Africa katika kuchangia uwepo wa usalama wa chakula Kwa ngazi za Taifa na Bara na ushiriki wa vijana na  wanawake" Amesisitiza Waziri Bashe.

Bashe amesema kuwa Mkutano Wa AGRF Mwaka huu 2023 unafungua Milango ya Matumizi ya Ubunifu  katika kuimarisha kilimo pamoja na kufungua Milango ya uwekezaji zaidi itakayohakikisha uwepo wa ubunifu,utungaji wa sera Bora pamoja na uwekezaji kwenye sekta ya kilimo.

"Wakati tukiendelea na jitihada za kuliwezesha bara la Africa  kuwa kitovu cha usalama wa chakula Duniani, tunapaswa kuwapa kipaumbele vijana na wanawake katika harakati hizi kutumiwa uwezo wao Wa ubunifa na ufanyakazi  unaoweza kuchangia Maendeleo na uhakika wa upatikanaji wa chakula Cha uhakika na salama" Amesema Bashe.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Wa jukwaa hilo Bw.Amath Pathe Sene amebainisha kuwa ubunifu,Sera Bora, uwekezaji wa kimkakati ni njia sahihi katika kuhakikisha upatikanaji Wa Mifumo imara ya chakula.

"AGRF 2023 itahusisha programu mbalbali kati ya wadau ambapo watapata wasaha wa kujadiliana na kubadilishana uzoefu,ubunifu na Mbinu mbalimbali wanazotumia katika kutekeleza shughuli za kilimo pamoja na septemba 3,2023 wageni wa mkutano watapata wasaha wa kutembelea na kujionea shughuli za kilimo zinazofanywa na watanzania na kujionea Mafanikio Mbalimbali yaliyofikiwa" Amesema Bw Sene.




Post a Comment

Previous Post Next Post