ZAIDI YA JUMBE 84,000 ZA SIMU ZIMETUMWA KWA WADAIWA WA KODI YA PANGO LA ARDHI.



Waziri Wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt.Angeline Mabula akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Maboresho yaliyofanyika kwenye Mifumo unaowezesha wamiliki wa Ardhi kupokea ujumbe kupitia simu za Mkononi.


WIZARA ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi imefanya maboresho katika mfumo mzima wa utunzaji kumbukumbu za ardhi, utozaji wa kodi na utoaji wa huduma za Sekta ya Ardhi Kwa lengo la kuwakumbusha Wananchi kulipa Kodi Kwa wakati kupitia simu za viganjani.

Akizungumza Leo Jijini Dodama April 21.2023,kuhusu Maboresho Yaliyofanyika kwenye Mifumo Unaowezesha Wamiliki wa Ardhi kupokea Ujumbe Kupitia Simu za Mkononi,Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula amesema kuwa ujumbe unaotumwa kwa sasa umeainisha jina la mmiliki, taarifa za kiwanja,(namba ya kiwanja, kitalu na eneo la kiwanja kilipo), namba ya utambulisho ya mlipa kodi (lot ID), kiasi cha kodi  inayodaiwa, riba itayosamehewa, deni la msingi  na control namba ya kulipia deni husika.

"Hadi sasa zaidi ya jumbe 84,000 za simu zimetumwa kwa wadaiwa wa kodi ya pango la ardhi zikiwa na deni la msingi kiasi cha takribani bilioni 115 ambazo zinatarajiwa kukusanywa katika mikoa 25" amesema Dkt Mabula.

Aidha, Dkt Mabula Amesema kwa mkoa uliobaki ambao ni Dar es Salaam zoezi hili linaendelea na ifikapo tarehe 30 Aprili, 2023 wamiliki wa ardhi katika mikoa yote ya Tanzania Bara watakuwa wametumiwa jumbe kupitia simu za mkononi kuhusiana na madai ya kodi ya pango la ardhi.  

"Hatua hii inatarajia kuongeza mapato ya yanayotokana na sekta ya Ardhi na matarajio yetu kuwa zoezi hili litakuwa endelevu na litatekelezwa sambamba na kuendelea na maboresho ya mifumo na Naomba nitoe taarifa kwa wananchi wote kuwa wakiona ujumbe katika simu ukianza na neno ardhi wajue ni jumbe sahihi na zinatoka Wizara ya Ardhi zikiwakumbusha kulipa kodi kwa wakati ili wanufaike na msamaha uliotolewa na Mhe.Rais Dkt. Samia Suruhu Hassan na mwisho wa Msamaha ni tarehe 30 Aprili 2023" Amesema Dkt Mabula.

Sambamba na Hayo,Dkt Mabula amewakumbusha Wamiliki wa Ardhi kulipa Kodi ya pango la Ardhi na endapo hawatafanya hivyo Wizara itachukua hatua za kisheria ikiwemo kuwafikisha mahakamani wadaiwa wa kodi ya pango la ardhi ili kufidia kodi husika au kupendekeza ubatilisho wa milki kama masharti ya umiliki yanavyojielekeza. 

"Awamu ya kwanza ilianza Julai, 2022 hadi tarehe 30 Disemba na awamu ya pili ilianza Januari, 2023 na itafikia ukomo tarehe 30 Aprili, 2023,Baada ya muda huo kupita, Wizara itachukua hatua za kisheria ikiwemo kuwafikisha mahakamani wadaiwa wa kodi ya pango la ardhi ili kufidia kodi husika au kupendekeza ubatilisho wa milki kama masharti ya umiliki yanavyojielekeza,

Natoa wito kwa wamiliki wa ardhi wenye madeni kuchangamkia nafuu iliyotolewa na Mhe. Rais ya kulipa madeni yao ya msingi ili wasemehewe riba ndani ya muda uliotolewa. Amesema Dkt Mabula.

Ikumbukwe kuwa katika Mwaka wa Fedha 2022/23, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassani alitoa msamaha wa riba ya malimbikizo ya pango la ardhi ambapo wananchi walio na malimbikizo wamepewa nafuu ya kulipa deni la msingi ili wasamehewe riba ya malimbikizo kuanzia Julai 2022 hadi Machi, 2023 ambapo Katika kipindi hicho, jumla ya wamiliki 9,188 walinufaika na msahaha huo ambapo shilingi bilioni 32 zilikusanywa ikiwa ni deni la msingi na shilingi bilioni 21.9 zilisamehewa ikiwa ni riba ya malimbikizo ya kodi ya pango la ardhi.

Post a Comment

Previous Post Next Post