MAUDHUI YASIYOFAA MTANDAONI NI MOJA YA CHANZO CHA KUFANYIWA UKATILI WA KIMTANDAO
Watoto walio chini ya umri wa miaka 18 wameaswa kuwa makini na maudhui wanayochapisha mtandaoni ili kujiepusha kufanyiwa ukatili kwa njia ya mtandao.
Afisa Maendeleo ya Jamii Bw. Amos Mpili kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum amesema kabla ya kupiga picha au video yenye maadili yasiyofaa mtoto mwenyewe anapaswa kujiuliza kama mzazi, mlezi au jamii ikiziona zitakuwa zinatoa ujumbe gani.
Amesema kuwa kwa kupiga na kuposti picha zenye maudhui yasiyofaa katika jamii wanajiweka katika hatari ya kufanyiwa ukatili wa kimtandao.
Sambamba na hilo amewaasa watoto kutoweka taarifa zao binafsi na za familia zao kwenye mitandao ya kijamii ili kujiepusha na hatari ya kufanyiwa ukatili wa watoto mtandaoni au uhalifu wa mtandaoni.
#UsalamawaMtotoMtandaoniJukumuLetuSote#