KURA ZA SIRI ZABAINI WAHALIFU DODOMA.
Wananchi wa Kata ya Kizota Jijini Dodoma wametakiwa kuweka utaratibu wa kujitambulisha kwa viongozi wa mitaa ikiwemo mabalozi, Jambo ambalo litasaidia kuwabaini wahalifu wa ndani na nje katika jamii.
Kauli hiyo imetolewa September 04, 2024 na Mkuu wa Polisi Jamii Dodoma Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Eva Stesheni wakati alipofika na Polisi kata wa Wilaya ya Dodoma Mjini kutoa pole kwa familia iliyofanyiwa ukatili dhidi ya mtoto na kuzungumza na wakazi wa Kizota.
Aidha Stesheni amesema kumekuwa na kasumba ya wananchi kuhamia na kukaribishana kiholela katika mitaa bila kuwa na utambuzi sahihi kwa viongozi pamoja na wananchi jambo ambalo hupelekea uhalifu kufanyika kwa kukaribisha watu na kutokujua shughuli wamazofanya au kuwa na taarifa sahihi.
Stesheni amewasihihi wananchi hao kukemea vitendo vya ukatili vinavyofanywa na baadhi ya wananchi wasiokuwa na maadili nakuleta taswira mbaya kwa Mkoa wa Dodoma hivyo amewataka wazazi pia kusimamia malezi ya watoto na kufatilia mienendo yao kwa ukaribu.
Vile vile wananchi wa kata ya Kizota Mbuyuni wamelipongeza Jeshi la Polisi kwa kuendesha zoezi la upigaji wa kura za siri ili kubaini baadhi wahalifu ambao hujishughulisha na vitendo viovu. Katika jamii.
Hata hivyo Jeshi la Polisi Mkoa Wa Dodoma kupitia kampeni ya familia yangu haina mhalifu imeweka kambi katika eneo la Kizota kupitia Polisi Kata hao ili kutoa msaada wa kielimu juu ya masuala ya ulinzi na usalama kwa wananchi.