HOSPITAL YA TAIFA YA AFYA YA AKILI MIREMBE SIYO HOSPITAL YA VICHAA-DK. LAWALA


HOSPITAL YA TAIFA YA AFYA YA AKILI MIREMBE SIYO HOSPITAL YA VICHAA-DK. LAWALA

Na,Saleh Lujuo-Dodoma

MKURUGENZI Mtendaji  Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe Dr. Paul Lawala, amekemea kwa vikali vitendo vya baadhi ya watu kusema Hospital hiyo ni ya vichaa jambo ambalo siyo sawa na watu wengi hushindwa kuwapeleka wagonjwa hospitalini hapo.

Akizungumza leo Agosti 30,2024 jijini Dodoma, wakati akifungua mafunzo ya Afya ya Akili kwa kuwajengea uwezo  waandishi wa habari  juu ya kuandika habari zinazohusu changamoto ya Afya ya Akili ambapo amesema kuwa jamii haitambui kuhusu hospital hiyo jambo ambalo wamejijengea vichwani mwao kwamba hospital hiyo ni yavichaa.

Mkurugenzi huyo Dr. Paul Lawala ,amesema waandishi wa habari, wanajukumu kubwa la kuhakikisha kuwa jamii inatambua na kuthamini afya ya akili na kuacha dhana potofu ya kushinda kuwapeleka wagonjwa hospitalini hapo kwani hospitali hiyo inatoa huduma za kisaikolojia pamoja na matibabu ya changamoto Mbalimbali za kiafya zinazomkabili binadamu.

"Hospital hii inatibu magonjwa Mbalimbali pamoja na kutoa ushauri wa kisaikolojia kwa watu ambao wanachangamoto ya Afya ya akili,na hii hospital inawasaidia watu wengi sana hususani mtu alietumia Madawa ya kulevya akifika hapo anapatiwa ushauri na anakaa sawa kabisa". Amesema Dk. Lawala

Sambamba na hayo amewasisitiza waandishi wa Habari kuwaelimisha watanzania katika kuhakikisha wanafahamu umuhimu na dhamira ya hospital hiyo katika kutoa huduma za kuwahudumia wananchi.

"lengo la mafunzo haya kwa waandishi wa habari ni kuboresha uelewa na ujuzi kuhusu masuala ya afya ya akili kupitia mawasilisho yatakayofuatiwa na mijadala , ili watoe taarifa sahihi kwa jamii kupitia vyombo vya Habari." Amesema

Akizungumzia kuhusu umuhimu wa mafunzo hayo amesema afya ya akili ni sehemu muhimu ya afya ya jumla ya mtu binafsi na jamii kwa kuwa Afya ya Akili ni Afya,Afya ya akili inamhusu kila mtu na hakuna afya bila afya ya akili.

"Kumekuwa na hali ya unyanyapaa na ubaguzi dhidi ya wale wanaopambana na changamaoto za Afya ya Akili na magonjwa ya akili". Amesema

Ameongeza kuwa :”Tunataka kuhakikisha kwamba mnakuwa na uwezo wa kutambua habari sahihi, kuzuia kusambaza habari zilizopotoshwa, na zaidi ya yote, kuweza kutoa taarifa kwa njia ambayo inaondoa unyanyapaa na kuongeza uelewa katika jamii,”.

Afya ya akili inahusu mtu anavyofikiri, anavyohisi na anavyotenda pamoja na ile inayomuwezesha mtu,kujitambua kuhusu uwezo, vipaji na hata udhaifu wake, kujifunza, kufanya anachopenda na asichopenda pamoja na kidhibiti na kuhimili changamoto za kawaida za kimaisha.

Post a Comment

Previous Post Next Post