ELIMU YA AFYA KUHUSU UGONJWA WA MPOX YATOLEWA KWA WANAFUNZI MSALATO


ELIMU YA AFYA KUHUSU UGONJWA WA MPOX  YATOLEWA  KWA WANAFUNZI  MSALATO.

Na. Elimu ya Afya kwa Umma.

Wanafunzi  wa kike kutoka shule ya Sekondari ya Wasichana Msalato  Mkoani Dodoma wamepewa elimu ya afya kuendelea kuchukua tahadhari kuhusu ugonjwa wa Mpox.

Akitoa elimu hiyo wakati wa zoezi la kukabidhi taulo za kike  kwa shule ya  Sekondari ya Wasichana Msalato Mkoani Dodoma  Beauty Mwambebule kutoka Wizara ya Afya, Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma ametoa wito kwa wanafunzi kuwa na desturi ya kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni mara kwa mara, kuepuka misongamano.

“Tuache tabia za kusalimiana kwa kushikana mikono na tunawe mikono yetu mara kwa mara kwa maji tiririka na sabuni ” amesema .

 Aidha, ametaja dalili za ugonjwa huo kuwa ni pamoja na kuumwa kichwa, kutokea vipele sehemu mbalimbali za mwili huku akisisitiza umuhimu wa kutoa taarifa kupitia namba 199 .

Post a Comment

Previous Post Next Post