WMA YAAGIZWA KUPIMA MITA ZA UMEME KABLA HAZIJAFUNGWA KWA WANANCHI
Na,Saleh Lujuo-Dodoma
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jaffo (Mb) ameiagiza Wakala wa Vipimo nchini (WMA) kuhakikisha wanapima mita za umeme kabla hazijaenda kufungwa kwa wananchi.
Dkt. Jaffo ametoa maagizo hayo leo Jijini Dodoma Julai 17,2024 alipotembelea ujenzi wa ofisi kuu ya wakala wa vipimo ambapo amewataka wakala hao kukamilisha Ujenzi wa jengo hilo kwa ubora na Kwa wakati.
"Endeleeni kufanya kazi kwa Weledi na mkakague maeneo yote ambayo yanatakiwa yafanyiwe ukaguzi hususani katika mita za umeme kabla hazijaenda kwa walaji". Amesema waziri Jaffo.
"Kufanya hivyo ni kuwapunguzia gharama wananchi kwa kufungiwa mita ambayo haina ubora na mwisho wa siku kulipa bili isiyo sahihi". Ameongeza
Mbali na hayo Waziri Dkt.Jaffo amewapongeza wataalam wa Wakala wa vipimo Tanzania kwa kutumia mapato ya ndani kujenga jengo hilo na kwa kufanya hivyo ni kutekeleza maagizo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Kwa upande wake Joseph Maliti ambaye ni Mwakilishi wa Mtendaji Mkuu wa wakala wa vipimo amesema wakala wa vipimo imepokea maelekezo yote yaliyotolea na waziri jaffo ambapo wameahidi watafanya kazi na kuhakikisha jengo hilo linakamilika kwa wakati.
"ujenzi wa jengo hili unagaharimu kiasi cha Shiling Bilioni 6, na mpaka sasa ujenzi umefikia asilimia 81.5 na kazi nyingi zilizobaki mpaka sasa ni za nje ikiwemo Mashimo ya kuhifadhia maji taka". Amesema
"ujenzi wa jengo hili unagaharimu kiasi cha Shiling Bilioni 6, na mpaka sasa ujenzi umefikia asilimia 81.5 na kazi nyingi zilizobaki mpaka sasa ni za nje ikiwemo Mashimo ya kuhifadhia maji taka". Amesema
Naye Mhandisi Justin Kyando ambaye ni Mhandisi wa Kampuni ya Ujenzi ya Mohammed Builders amesema kazi zilizosalia ni chache ukilinganisha na muda uliobaki ambapo wanatakiwa kukabidhi jengo hilo ifikapo Januari 2025.
Ujenzi wa jengo la wakala wa vipimo unagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 6.17 na Ujenzi huo unatarajiwa kukamilika ifikapo Januari 2025.