UHURU WA KUJIELEZA NI HAKI ZA BINADAMU-NYABIRI
Na,Saleh Lujuo-Dodoma
Makamu wa Rais wa Tanganyika law society Deus Nyabiri amesema uhuru wa kujieleza ni haki za binadamu pamoja kupata habari na kuisambaza kwani haki ya kujieleza na haki ya kupata habari ni jambo kubwa.
Hayo yamesemwa Leo hii jijini Dodoma na Makamu wa Rais wa Tanganyika Law Society Deus Nyabiri wakati akifungua Mafunzo ya utoaji Elimu ya kuwajengea uwezo wahariri wa vyombo vya habari nchini.
Na kuongeza kuwa hapa nchini Kuna vyombo vingi vinavyotoa habari hivyo ni wajibu wa TLS kuwajengea uwezo watoa habari wa vyombo hivyo.
"Katika katiba Kuna swala la haki za binadamu Moja wapo ni haki ya kujieleza, haki ya kupata habari, haki ya kujieleza ni jambo kubwa lakini haki ya kupata habari na kuisambaza pia ni jambo kubwa tunavyo vyombo vya habari mbalimbali vinazotoa taarifa kwa jamii kuhusu mambo mbalimbali hivyo ni wajibu wa Tanganyika low society kuwapa Elimu wanatoa taarifa ya maendeleo ya nchi Ili kuwajengea uwezo " amesema Nyabiri.
Aidha Nyabiri amesema kuwa anaamini Katika mafunzo Hayo kila mwana taaluma atatoka na kitu chanya ambacho kitamsaidia Katika kuchanganua habari zinazofaa na zisizofaa Katika jamii.
" Imani yangu ni Moja kuwa kila aliyekuwa hapa atatoka na elimu ya kutosha lakini namna ya kunitumia Elimu hiyo ndo changamoto kwa sababu anaweza kupata Elimu lakini mtu anaweza kuingia hisia au Mihemko ya kibinadamu akaleta kitu tofauti lakini hapa tunaamini watapata kitu chanya Cha kunisaidia kujua kuwa habari hii inafaa Katika jamii au habari hii jamii haiwafai" Amesema Nyabiri.
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Tathimini na ufatiliaji TLS Seleman Pingoni amesema kuwa semina hii imekuwa ikitolewa kwa sababu kulikuwa na malalamiko ya kutolizishwa Katika swala la utoaji wa haki.