MFUMO WA NeST KUONDOA VITENDO VYA RUSHWA KWENYE UNUNUZI WA UMMA

 


MFUMO WA NeST KUONDOA VITENDO VYA RUSHWA KWENYE UNUNUZI WA UMMA

Na,Saleh Lujuo-Dodoma

Licha ya uwepo wa Sheria,kanuni, Miongozo na taratibu za kusimamia na kuendesha ununuzi wa umma nchini,Bado kumekuwepo na changamoto mablimbali ikiwemo matumizi yasiyoridhisha ya Fedha za umma kwenye ununuzi wa umma ikiwemo gharama kubwa katika kununua bidhaa,kazi na huduma mbalimbali ukilinganisha na bei za soko.

Aidha,Serikali imewataka wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenda kutoa elimu kwa wananchi kuhusu mfumo mpya wa ununuzi wa umma wa kielektroniki ujulikanao kama NeST ili kuondoa urasimu na kukuza uwazi. 

Kauli hiyo ya serikali ameitoa Naibu waziri Ofisi ya waziri mkuu Kazi,Ajira,vijana na watu Wenye ulemavu Patrobas katambi kwa niaba ya waziri wa Fedha katika semina ya Wabunge iliyoandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) Bungeni Dodoma ambapo amesema mfumo huo ni tiba na imara kwani itasaidia kuleta maendeleo kiuchumi na kupiga Vita ufisadi. 

Naye Mkurugenzi Mkuu wa PPRA Eliakimu Maswi alisema  Sheria Mpya ya Namba 410  ya Ununuzi wa Umma itaanza kutumika tarehe 17 mwezi Juni huku Kanununi kuanza kutumika Julai 1 mwaka huu 2024


"PPRA imepewa jukumu la kufanya ukaguzi wa masuala ya ununuzi na ugavi kwa lengo la kuhakikisha kuwa mikataba ya ununuzi na ugavi inatekelezwa kwa mujibu wa Sheria". Amesema Maswi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kwimba Bi. Happiness Msanga ambapo Halmashauri hiyo imekuwa kinara wa kutumia mfumo wa NeST  na ametaja kwa nini wamefanikiwa pamoja na faida walizozipata ni kwamba  walianza kutoa elimu Kati ya wadau wa ununuzi na watumishi wa serikali . 

PPRA imepewa jukumu la kuandaa bei kikomo kwa baadhi ya bidhaa, huduma na kandarasi zenye viwango na vigezo vya kiufundi lengo likiwa ni serikali kununua bidhaa,huduma na kazi za ujenzi kulingana na bei ya soko.


Post a Comment

Previous Post Next Post