KITUO CHA KIMAREKANI KIMEZINDULIWA DODOMA KWA LENGO LA KUTOA HUDUMA YA KOMPYUTA NA INTANETI BURE


KITUO CHA KIMAREKANI KIMEZINDULIWA  DODOMA KWA LENGO LA KUTOA HUDUMA YA KOMPYUTA NA INTANETI BURE

Na,Saleh Lujuo-Dodoma

Naibu waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Omary Juma Kipanga amezindua kituo Cha kimarekani katika eneo la Uhindini ndani ya Maktaba kuu ya Dodoma chenye lengo la Kutoa huduma za kompyuta na internet bila malipo yoyote ili Jamii inufaike na huduma hiyo.

Akizungumza Mara baada ya kuzindua kituo hicho jijini Dodoma,Naibu waziri huyo ameishukuru serikali ya Marekani kwa msaada huo ambapo ameitaka Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania kuhakikisha vifaa vilivyotolewa vinatunzwa.

Kwa upande wake Karen Nasso Mtaalamu wa Vituo vya Kimarekani amesema vituo vya Kimarekani ni vituo vinavyowekwa katika maeneo mbalimbali ya kijamii ili Jamii ujifunze vitu Mbalimbali kulingana na mahitaji yao.

Awali Dkt Mboni Amiri Ruzegea Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania amesema kituo hicho kitahudumia watu wote hususani wanafunzi wa ngazi zote za Elimu.

Kituo cha Kimarekani Uhindini Dodoma ni kituo Cha Tano kufunguliwa nchini ikiwa ni Mtandao zaidi ya vituo Millioni 60 Duniani.


Balozi wa Marekani Michael Battle Akizungumza kuhusu umuhimu wa kituo hicho.


Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mjini  Jabiri Shekimweri Akizungumza katika Uzinduzi huo.










Baadhi ya washiriki waliohudhuria Uzinduzi huo

Post a Comment

Previous Post Next Post