WATUMISHI WA WIZARA YA FEDHA KUTOKA VISIWANI ZANZIBAR NA TANZANIA BARA WAIGUSA JAMII KWA KUTOA SADAKA KATIKA VITUO VYA WATOTO WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU.

WATUMISHI WA WIZARA YA FEDHA KUTOKA VISIWANI ZANZIBAR NA TANZANIA BARA WAIGUSA JAMII KWA KUTOA SADAKA KATIKA VITUO VYA WATOTO WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU.

Na,Deborah  Lemmubi-Dodoma.

Watumishi wa Wizara mbili  za fedha kwaTanzania Bara na Visiwani Zanzibar wametembelea Vituo vya kulelea Watoto wanaoishi katika Mazingira magumu kwa wilaya ya  Dodoma mjini ikiwemo kituo cha Safina kilichopo Ntyuka na kituo cha Asmaa Bint Shams kilichopo kisasa,na wilaya ya Chamwino kituo cha wasiona watu wazima Buigiri na shule ya msingi Buigiri kwa watoto wenye mahitaji maalum, na kuweza kutoa Sadaka ya vitu mbalimbai ikiwemo vyakula,sabuni,mafuta,dawa za meno,fedha na mahitaji mengine kwa wahitaji hao.

Mara baada ya kumaliza ziara hiyo katika vituo vyote vinne Wito ukatolewa kwa wakuu na walezi wa watoto hawa kuwalea na kuwasimamia watoto ili waje kuwa watoto wema katika Taifa.

Wito huo wa kuwalea na kuwasimamia watoto umetolewa na Bwana Rajab Uweje ambaye ni Afisa Uendeshaji kutoka Ofisi ya Raisi fedha na Mipango Zanzibar wakati akizungumza mara baada ya kutoa Sadaka katika vituo huvyo ndani ya  wilaya ya Dodoma mjini na wilaya Chamwino.

Na kuongeza kuwa wametoa ahadi kwa walezi hao kuwa wamechukua  changamoto zilizopo katika vituo na watazipeleka kwa uongozi wao na endapo watafanikiwa kuwashawishi watarudi kuona namna wanavyoweza kuwasaidia tena.

"Wito wangu kwa walezi wa vituo waendelee kuwatunza watoto hawa,kuwasimamia vizuri ili wawe wazuri kwa Taifa la leo na wawe Raia wema wa baadae"

"Na tumetoa ahadi kuwa tumechukua zile changamoto zao ili tuone tunaenda kuzifanyia kazi vipi,endapo tutafanikiwa kuwa shawishi viongozi wetu katika Taasisi zetu basi tutarudi kuina tutawasaidia vipi"

Bwana Mugusi Musita ambaye ni Mwenyekiti wa Hazina Sports club amewaomba viongozi wake ni waone ni namna gani wanaweza kuwashika mkono wahitaji waliopo katika vituo hivi na vingine vingi vyenye uhitaji.

"Ujumbe wangu kwa viongozi wetu ni kwamba waone ni namna gani wanaweza kusapoti hivi vituo kwani vina mahitaji mengi kweli kweli,tunashukuru tumewapa chochote lakini bado hakitoshi".

Mratibu wa kituo cha Safina Street Net work kilichopo Ntyuka Bwana Ebenezer Ayo kwanza amewashukuru watumishi hao wa Wizara ya fedha kwa kuwatembelea na kutoa misaada katika kituo Chao,na kuiomba jamii kushiriki kujitoa katika kuwalea watoto wanaoishi katika Mazingira magumu na kuacha kuwapa pesa wakiwa mtaani kwani kwa kufanya hivyo wanachochea watoto kuendelea kubaki mtaani badala ya kwenda katika vituo vya malezi.

"Mimi wito wangu kwa jamii ni kuwakmba kuacha ule utaratibu wa kuwapa watoto hela waliopo mtaani kwa kwa kufanya hivyo wanafanya watoto waendelee kuona ni sawa kukaa mtaani badala ya kuja katika vituo vya malezi ".

Katika kituo cha Asmaa mratibu wa Dhi Nureyn Taifa kutoka kituo cha Asmaa Bint Shams Dodoma Bwana Muhibu Mtahu amesema kuwa yeye anaamini kuwa sehemu salama namsingi katika malezi ya mtoto ni katika familia ikitokea mtoto  akaenda katika kituo cha malezi basi mambo yawe yamekaa vibaya sana kwani kuna tofauti kwa mtoto anayelelewa nyumbani na familia na anayelelewa katika kituo cha malezi.

"Kama ilivyo Serikali ndivyo tulivyo Waislamu kuwa tunahimiz watoto walelewe katika familia,msingi wa kwanza na sehemu sahihi zaidi ya mtoto ni kwenye familia. Tunamuweka mtoto kwenye kituo pale ambapo tunaona kila kitu hakiko sawa na tunapomuweka kwenye kituo hatumaanishi kuwa atakaa moja kwa moja".

Pia wametembelea katika kituo cha wasioona watu wazima kilichopo kijiji cha Matembe Bora Buigiri ambapo Mwenyekiti wa wasioona Bwana Yaledi Daudi kuiomba Serikali kuwaunga mkono katika kuwaboreshea makazi yao kwani yamekuwa ni ya muda mtefu ili na wao wawe na makazi bora.

"Natoa ombi kwa Serikali kwamba tuaomba makazi yetu yamekuwa ni ya muda mrefu, hivyo tunaiomba Serikali ikatushika mkono ikatuyengenezea nyumba bora ili na sisi tuwe na makazi bora".

Katika Shule ya Msingi ya watoto wenye mahitaji maalumu wakiwemo watoto wenye ulemavu wa ngozi,wasioona na wenye uoni hafifu Mkuu wao wa Shule  Bwana Samweli Jonathan ameiomba Serikali kuwasaidia katika kuboresha miundombinu ya kupikia ya gesi ili na wao waingie katika utunzaji wa Mazingira kwa kuondokana na matumizi ya kuni.

Haya ni moja kati ya mambo mengi mbalimbali waliyoyafanya Watumishi wa Wizara ya fedha katika wiki hili la pasaka ambapo ilitanguliwa na Tamasha la michezo.

Post a Comment

Previous Post Next Post