HALMASHAURI AMBAZO HAZITUMII MFUMO WA NeST TUTAWAPELEKA MAHAKAMANI-BW. MASWI
Na,Saleh Lujuo -Dodoma
Mamlaka ya Udhibiti wa ununuzi wa Umma (PPRA) imekiri kuwa Kati ya Halmashauri zote 184 nchini ni Halmashauri 6 tu,sawa na Asilimia 3.3 ya Halmashauri zote ndizo ambazo zimeanza kutumia Mfumo mpya vizuri wa Kielektronic wa NeST ambapo baadhi ya Halmashauri za Miji Bado hazijatumia kabisa Mfumo huo.
Hayo yamebainishwa leo Novemba 23,2023 jijini Dodoma na Bw. Eliakim Maswi, Afisa Mtendaji Mkuu PPRA katika semina kazi kwa ajili ya kuhakikisha wakurugenzi wanazingatia sheria za manunuzi kupitia Mfumo wa ununuzi wa Umma ujulikanao kama NeST ili kudhibiti ununuzi wa Umma unaozingatia uwazi ambapo Halmashauri 115 hazina habari kama kunakutumia mfumo huo.
"Kuna Halmashauri 9 zenyewe zimekuwa kama hazijui kabisa kama kuna suala la kutumia mfumo, na hazijawahi kutumia mfumo huu kufanya manunuzi". Amesema
"hii ni hatari na hatuwezi kwenda hivi kabisa, unajua serikali Raha sana na hatuwezi kubembeleza kabisa na kwabahati nzuri sheria ya ununuzi iliyopitishwa imetupa madaraka ya kuwapeleka mahakani wale wote wanaokiuka Sheria , tutawapeleka mahakamani au kulipa sichini ya millioni kumi au miaka saba jela au vyote viwili". Ameongeza
Aidha, Bw. Maswi amesema Kwa Halmashauri ambazo hazitaki kutumia Mfumo huo wataadhibiwa kwa kitendo cha kutotumia mfumo kwani wanakiuka taratibu na Sheria zilizowekwa huku akizipongeza Halmashauri zilizofanya vizuri kwa kutumia Mfumo huo ikiwemo Halmashauri ya Wilaya ya Ngara.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI anayeshughulikia Serikali za mitaa na Tawala za Mikoa Sospita Mtwale amesema Mfumo huo utasaidia Serikali za Mitaa na halmashauri zote Nchini kufanya manunuzi kwa wakati ikiwa ni pamoja na kuendana na Mamlaka ya Serikali mtandao inayoelekeza matumizi na manunuzi yote ya serikali kufanywa kidigitali.
"Nitoe rai kwa Wakurugenzi wote nchini kuhakikisha wanazingatia maelekezo ya PPRA kwa ufasaha ,watakaokiuka tulishatoa maelekezo kwa mujibu wa sheria ya PPRA kuwafikisha mahakamani,tuna imani semina hii itasaidia wakurugenzi kurudi kwenye mstari na Manunuzi yote lazima yafuate utaratibu wa serikali". Amesisitiza
Serikali imekuwa ikiboresha mifumo ya manunuzi mara kwa mara kuendana na mabadiliko ya kidunia ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na kwa wakati ambapo wakurugenzi wote nchini wanakumbushwa kuhakikisha wanazingatia maelekezo ya PPRA kwa ufasaha na watakaokiuka maelekezo kwa mujibi wa sheria ya PPRA watafikishwa mahakamani.