WASHIRIKISHENI WANANCHI KUWA KITOVU CHA MAENDELEO KWA MASLAHI YA TAIFA- WAKILI MPANJU

 

WASHIRIKISHENI WANANCHI KUWA KITOVU CHA MAENDELEO KWA MASLAHI YA TAIFA- WAKILI MPANJU

Na,Saleh Lujuo-Dodoma 

Naibu Katibu Mkuu wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na makundi maalum Wakili Amoni Mpanju amefungua mafunzo ya mpango wa Taifa wa kuhamasisha na kusimamia maendeleo ngazi ya msingi kwa wataalamu wa ngazi ya kata Jijini Dodoma ambapo amewasihi  kuwashirikisha wananchi kuwa kitovu cha maendeleo kwa maslahi ya Taifa na watu wake.

Aidha amewataka Viongozi wataalamu ngazi ya kata kuhakikisha wanaweka mpango kazi unaopimika wa utekelezaji maendeleo ngazi ya masingi kwenye maeneo yao ili kuakisi  maudhui ya mpango wa kitaifa unaosimamia maendeleo.

Kauli hiyo imetoleo leo Jijini Dodoma na wakili Amon Mpanju katika Mafunzo ya Mpango wa Taifa wa kuhamasisha na kusimamia maendeleo ngazi ya msingi 2022/2023 hadi 2025/2026 ambapo amesema Mpango huo wenye lengo la kuhamasisha maendeleo ngazi ya msingi na kuwafanya wananchi kuwa kitovu cha maendeleo kwa kutumia rasilimali zilizoko kwenye maeneo yao utafanikiwa ikiwa watatoka ofisini kwenda kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua kwa wakati.

“Nawasihi mkawajibike kwa kufanya kazi zenye matokeo  kwa kuzingatia umoja na uzalendo kwa kushirikishana ngazi na kata kuheshimiana kwa taaluma mshirikishane ujuzi na maarifa mchape kazi kama timu ndo mtaweza kufikia nia ya watanzania kuwa kitovu cha maendeleo ngazi ya msingi,’’amesema.

Mpanju pia ameelekeza kuwa mpango kazi huo ufanyike na kila mtu kwenye eneo lake kwa kuwasilisha taarifa ya kina ya uwajibikaji wake namna anavyowahudumia wananchi ili kufanya tathmini kwa pamoja na kuweka mkakati wa maboresho ya kiutendaji.

"Mkiyaishi hayo tutakuwa na matokeo tarajiwa,mkahakikishe wananchi wanatoa ushirikiano ,muelewe huu mpango ni muhimu kwa Serikali hivyo mkautekeleze kwa vitendo,Kumbukeni Serikali imewagharamia mje mjifunze ili kuwaelimisha wananchi na kuwa na maendeleo ya pamoja ngazi ya msingi na taifa kwa ujumla,”ameeleza

Aidha, Wakili Mpanju amewataka washiriki hao kuwa makini na mijadala inayoendelea kwenye mafunzo hayo huku akiwatahadharisha  kuachaa na matumizi ya simu bila mpangilio ili kuondoka na mkakati mmoja wa kuleta mapinduzi ya fikra na kuwafanya wananchi wajitambue.

“Tunafahamu kwa muda mrefu sasa,utendaji wa ngazi ya msingi umekuwa hauleti tija inayotakiwa kutokana na uzembe wa kitaalam,hakikisheni mnabadilisha utaratibu wa kufanya kazi wasikilizeni wananchi wanataka nini kwa sababu ninyi ndio mabalozi wa Serikali hivyo mkahakikishe mnakuwa mabalozi wazuri katika kuisemea serikali wakati wote,” amesisitiza

Akiwasilisha utekelezaji wa mpango wa Taifa wa kuhamasisha na kusimamia maendeleo ngazi ya msingi kwa wataalam wa ngazi ya kata, Mratibu wa Mpango huo Maua Ngusa amesema lengo kuu la mpango huo ni kuchochea na kufanya mageuzi ya fikra,mitazamo na kiutendaji kwa timu ya watalamu kwa ngazi ya msingi ili kuboresha utendaji kazi na utoaji wa huduma kwa wananchi.

"huu ndio mpango kazi wetu ambapo mikakati ya utekelezaji wa mpango huu ni kuimarisha uwezo kwa wataalam wa serikali katika ngazi ya msingi Kwa kuwapa mafunzo, Fedha, vitendea kazi,na ofisi na mkakati huu utatekelezwa na wizara zote za kisekta zenye wataalam ngazi ya msingi". Amesema

Akitoa nasaha Kwa wataalam ngazi ya kata, Mkurugenzi wa maendeleo ya jamii wa wizara ya Maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake na makundi maalumu Patrick Golwike amewasihi wataalam hao kufanya kazi kwa weledi na ujuzi walionao ili kusudi wananchi wapate huduma zinazostahili na kuipenda serikali yao.


"nyie wataalam ndiye mnatakiwa kufanya watu waipende serikali yao,hivyo wajibikeni na siyo kuilalamikia serikali". Amesisitiza

Mafunzo ya Mpango wa Taifa wa kuhamasisha na kusimamia maendeleo ngazi ya msingi 2022/2023 hadi 2025/2026 kwa wataalam wa ngazi ya kata katika jiji la  Dodoma unalengo la kuchochea na kufanya mageuzi ya fikra,mitazamo na kiutendaji kwa timu ya watalamu kwa ngazi ya msingi ili kuboresha utendaji kazi na utoaji wa huduma kwa wananchi.

Post a Comment

Previous Post Next Post