HAKUNA MHALIFU ATAKAYE BAKI SALAMA KATIKA MIPAKA YA TANZANIA-DPP MWAKITALU
Na,Saleh Lujuo-Dodoma
Mkurugenzi wa mashtaka nchini DPP Sylvester Mwakitalu ametoa onyo kali Kwa wahalifu Katika mipaka ya Nchi ambapo amesema uhalifu Katika Nchi ya Tanzania haulipi.
Mwakitalu ametoa onyo hilo leo septemba 29,2023 jijini Dodoma wakati akifungua kikao cha Tathmini cha Menejimenti ya ofisi ya Taifa ya Mashtaka ,Ofisi ya Mkurugenzi wa upelekezi wa makosa ya jinai ,na Taasisi za kuzuia na kupana na Rushwa.
Pia amesema madhara yatokanayo na uhalifu,Rushwa na ufisadi yamekua na athari kubwa Katika jamii na kusababisha wananchi kukosa huduma wanazozita.
"vikao vya pamoja hivi vya wakuu wa mashataka, wakuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Mikoa na wakuu waeupelelezi Mikoa kutasaidia kwa kiasi kikubwa kutafuta suluhu ya changamoto zinazojitokeza Katika jamii hususani makosa ya Uhalifu,Ufisadi na Rushwa". Amesema.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) CP. Salum Rashid Hamduni amesema wataendelea kushirikiana kwa pamoja ili kuhakikisha haki, amani na usalama vinapatikana Katika jamii.
"Katika kutekeleza majukumu yetu ya kila siku tunagusa Moja Kwa Moja haki za wananchi,hivyo ninamna gani tunatakiwa tunaharakisha Masuala ya Uchunguzi na uendeshaji wa Mashtaka na hili ndiyo jambo jema". Amesema CP. Hamduni
Naye Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini Kamishna wa Polisi Ramadhani Kingai amesema ushirikiano ni jambo Muhimu sana Katika kuwatendea haki wananchi kwa mujibu wa sheria na kanuni zilizowekwa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
"Mashirikianoa haya tunataka kupeleka huduma kwa wananchi ziwe rahisi kuliko ambavyo tungeweza kufanya kila mmoja kivyake lakini pia tufahamu kwamba umoja ni nguvu na na utengano ni udhaifu". amesema
Kikao Cha Menejimenti, Wakuu wa Mashtaka,Wakuu wa Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa Mikoa na wakuu wa upelelezi Mikoa kinafanyika kwa siku tatu kwa lengo la kushirikiana kwa pamoja Katika kuwahudumia wananchi kwa haraka na kukomesha vitendo vya makosa ya Uhalifu, Ufisadi pamoja Rushwa.