VIJANA ONGEZENI JUHUDI YA ZIADA KATIKA WIGO WA KISHERIA ILI NCHI IWE NA AMANI KWA MIAKA MINGINE IJAYO-PROF. KUSILUKA

VIJANA ONGEZENI JUHUDI YA ZIADA KATIKA WIGO WA KISHERIA ILI NCHI IWE NA AMANI KWA MIAKA MINGINE IJAYO-PROF. KUSILUKA

Na,Saleh Lujuo-Dodoma.

Wanafunzi wa vyuo vikuu nchini wametakiwa kuweka jitihada za ziada katika masomo yao ili kulijenga Taifa la Tanzania kwa  kuongeza ujuzi katika masomo yao.

Kauli hiyo imetolewa katika chou kikuu cha Dodoma  na Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Lughano Kusiluka katika kuhitimisha mashindano ya sheria za kimataifa na haki za binadamu kwa wanafunzi ili kuwa wazalendo kwa taifa lao.

"hii nchi hii Bado inaendelea na inahitaji vijana ambao wanafanya kazi,wanaoongeza juhudi ya ziada katika kazi zao ili kuilinda nchi kwa misingi ya amani na utulivu kwa vizazi vijavyo na kwa sasa pia". amesisitiza Prof. Kusiluka.

Aidha, Prof. Kusiluka amewataka vijana kuipenda nchi yao kwa kwa kukazana kusoma masuala ya sheria ili nchi iwe na wasomi ambao watasimamia misimamo ya hali ya juu kwa maslahi ya watanzania.

Kwa upande wake wakili wa kujitegemea Kanali Aloyce Lazier amesema kuna haja kubwa ya kila kijana kujitambua kwa kuongeza bidii katika masomo yao ili kuwa na ushindani wa kimataifa.

Nao baadhi ya washidi wa mashindano hayo chuo Kikuu cha Dar es salaam na Chuo Kikuu cha Iringa akiwemo Naomi Kileo na Daniel Alphonce wamesemawatafanya vizuri zaidi na kuongeza wigo waekisheria pamoja na kuongeza upeo wakisheria zaidi ili kushinda mashindano ya kimataifa kwa Africa nzima ambayo yanatarajia kufanyika Arusha mwaka huu.

Mashindano hayo yameshirikisha vyuo vikuu nchini kwa lengo la kuwajengea uelewa wanafunzi hao kuhusu Sheria za Kimataifa na Haki za Binadamu wakati wa Majanga ya Vita.

Post a Comment

Previous Post Next Post