VIJANA NA WANAWAKE CHANGAMKIENI FURSA ZA KILIMO-PINDI CHANA.
Na,Saleh Lujuo-Dodoma.
Waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Balozi Pindi Chana amewataka vijana na wanawake kuchangamkia fursa za kilimo.
Waziri Pindi ameyasema hayo katika ufunguzi wa kongamano la zao la mtama maonyesho ya wakulima 88 nzuguni Dodoma wakati alipotembelea moja ya shamba la mahindi na kuwasihi wananchi haswa wanawake na vijana kuchangamkia fursa za kilimo ikiwa kilimo ndio uti wa mgongo wa Tanzania.Aidha amesema kuwa dhamira ya muheshimiwa Rais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha wanawake na vijana wanachangamkia fursa zilizopo kwenye sekta ya kilimo ikiwa ni ajenda ya kuwa mzalishaji mkuu wa chakula barani Afrika na baadae kusambaza duniani kote.
"Nimeambiwa kuwa haya ni Maonesho ya Kumi na Tano ya Kanda na Maonesho ya kumi na mbili ya Mashindano ya Mifugo Kitaifa yatafanyika mwaka huu. Maonesho na Sherehe za Nanenane huwa na kaulimbiu mahususi ya mwaka, ambapo kwa mwaka huu kaulimbiu iliyopambanuliwa ni ‘VIJANA NA WANAWAKE NI MSINGI IMARA WA MIFUMO ENDELEVU YA CHAKULA’. Kauli mbiu hii, imeandaliwa mahususi kwa kuzingatia umuhimu wa usalama wa chakula katika jamii ikianzia na kaya na kwamba wanawake na vijana ndio wanashiriki ipasavyo katika shughuli za uzalishaji na upatikanaji wa chakula" Amesema Waziri Mhe.Balozi Chana.
Aidha ameongeza kuwa sekta ya Kilimo inayojumuisha Mazao, Mifugo, Uvuvi na Misitu bado ni mhimili wa uchumi wa Tanzania, kwa sababu inaajiri zaidi ya asilimia 80 ya watanzania na kwa kuzingatia Malengo ya Maendelo ya Taifa ya kuwa nchi yenye Uchumi wa kati unaotegemea Viwanda, ninaamini Kilimo kikiboreshwa viwanda vyetu vitapata malighafi ya uhakika na kuimarisha masoko kwa wakulima wetu, hivyo kuwepo kwa ajira za kuaminika kwa vijana na watanzania kwa ujumla. Wastani wa ukuaji wa Sekta ya Kilimo unabadilika mwaka hadi mwaka kutokana na kilimo chetu kwa kiwango kikubwa, kutegemea Mvua ambazo zimekuwa zikinyesha kwa viwango na mtawanyiko unaotofautiana mwaka hadi mwaka. Kwa mwaka 2022 Sekta ya Kilimo ilikua kwa asilimia 3.9 ikilinganishwa na asilimia 4.9 ya mwaka 2020.
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa singida Mhe.Peter Selukamba amesema kama mkoa zao lao la kimkakati ni alizeti na mpka sasa wamefikia asilimia44% ya uzalishaji na kusambaza mikoa ya jirani ikiwemo singida, Dodoma na Manyara na ni zao ambalo linawainua wananchi kiuchumi.
Mikoa ya Dodoma na Singida ni maarufu kwa kilimo cha zao la mtama wa aina mbalimbali. Umaarufu huu, umechangiwa na hali ya hewa inayopatikana maeneo mengi ya mikoa hii kustawisha vizuri zao la mtama. Ni kwa mutadha huo, Mtama ni zao linalohimizwa kuzalishwa kwa ajili ya uhakika wa usalama wa chakula na kipato kufuatia kuongezeka kwa uhitaji wa zao hili hapa nchini na nchi Jirani kama Burundi, Ruanda, Southern Sudan na Kenya.