BODI YA MKONGE IMEDHAMIRIA KUONGEZA UZALISHAJI WA TANI 120,000 KWA MWAKA IFIKAPO MWAKA 2025/2026


BODI YA MKONGE IMEDHAMIRIA KUONGEZA UZALISHAJI WA TANI 120,000 KWA MWAKA IFIKAPO MWAKA 2025/2026


Na,Saleh Lujuo-Dodoma.

Imeelezwa kuwa Tanzania ni Nchi ya pili Duniani kwa Uzalishaji wa zao la Mkonge ikiachiwa na Nchi ya Brazil ambayo ndio namba moja ambapo imepelekea Serikali kuweka hamasa kwa wakulima wadogo wa zao hilo.

Haya yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Mkonge Tanzania TSB) Bwana Saddy  Kambona leo jijini Dodoma wakati akielezea utekelezaji wa majukumu ya Bodi hiyo na mwelekeo wake wa utekelezaji kwa mwaka wa fedha 2023/24.

Aidha Mkurugenzi huyo amesema hadi mwaka 2020, TSB iliweza kusajili wakulima wadogo 6,887na Mwaka 2022, idadi ya wakulima wadogo waliosajiliwa ni 8,972.

"Hata hivyo, wakulima wadogo wa Mkonge ambao hawajafikiwa na kusajiliwa na TSB wanakadiriwa kufikia 22,000". amesema 

Sambamba na hayo Kambona amesema 
Kutokana na hamasa kubwa ya kilimo cha Mkonge iliyofanywa na Serikali, imepelekea kuongezeka kwa mashamba ya kulima Mkonge hasa kwa wakulima wadogo.

 "TSB imegawa mashamba kwa wakulima 983 wilayani Korogwe na wakulima wengine zaidi ya 3,000 wamegawiwa mashamba wilayani Kilosa na zoezi bado linaendelea". amesema.

"Pia, imepelekea kushusha riba kwenye mabenki ya biashara kwa mikopo inayoelekezwa kwenye kilimo, kununua mitambo mipya ya kuchakata Mkonge na kufufua mitambo ya kuchakata Mkonge ya Mashamba ya Kibaranga wilayani Muheza, Tanga na shamba la Serikali la TPL lililopo Kata ya Bwawani wilayani Arumeru, Arusha ambalo linasimamiwa na kuendeshwa na TSB". ameongeza.

Zao la Mkonge lilitangazwa kuwa ni zao la kimkakati mwaka 2019 na ni zao la Saba katika orodha ya mazao ya kimkakati hapa Nchini.

Post a Comment

Previous Post Next Post