MFUMO MPYA WA UNUNUZI WA UMMA KWA NJIA YA MTANDAO NeST KUANZA KUTUMIKA NCHINI
Na,Saleh Lujuo-Dodoma
Kutokana na mahitaji mapya ya teknolojia ya kuimarisha eneo la ununuzi wa Umma nchini,Serikali kupitia Mamlaka ya udhibiti wa ununuzi wa Umma nchini PPRA imetangaza kuanza Rasmi kutumika Kwa Mfumo Mpya wa ununuzi kwa njia ya Mtandao NeST.
Akizungumza Leo Jijini Dodoma Mwenyekiti wa Bodi hiyo Dr.Leonada Mwagike amesema sababu kubwa iliyopelekea ujenzi wa mfumo wa NeST ni hitaji la kuhakikisha ununuzi wa umma unazingatia Misingi mikuu ya Kimataifa katika ununuzi wa umma ambayo ni uwazi, usimamizi mzuri wa fedha za umma, Kuzuia mwenendo mbaya,ukidhi na Ufuatiliaji na uwajibikaji na udhibiti.
"hatua hii pia imezingatia na ongezeko la mahitaji katika matumizi ya mifumo ya TEHAMA ndani ya sekta" ameongezea Dr.Leonada
"Mfumo huu Wa NeST utakuwa Mbadala Wa Mfumo unaotumika hivi Sasa wa TANePS ambao unatarajiwa kutatua changamoto kadhaa za kiufundi na kukidhi mahitaji ya Serikali Katika sekta ya Ununuz ambapo ujenzi wa mfumo wa NeST ulianza Rasmi Tarehe 18 Julai,2022,Hadi kufikia mwezi juni 2023 Moduli muhimu Kwa ajili ya Kuruhusu Mfumo kuanza kutumika zimeshakamilika" amesema
Aidha, Dr.Mwagike amesema Mamlaka hiyo imeandaa mpango kabambe wa mafunzo ambapo hadi kufikia Tarehe 1 oktoba 2023 Taasisi zote za umma zitakuwa zimeshapatiwa mafunzo, zimesajiliwa na kuanza kutumia Mfumo Wa NeST.
"Utaratibu umewekwa ili Taasisi ambazo hazijapatiwa mafunzo ziweze kuendesha ununuzi wake Kwa kutumia Mfumo uliopo Kwa kipindi hiki Cha mpito Cha miezi mitatu ambapo Mamlaka inapenda kuufahamisha kuwa TAASISI NUNUZI ZOTE HAZITARUHUSIWA KUENDESHA MICHAKATO YA UNUNUZI NJE YA MFUMO WA NeST KUANZIA TAREHE 1 OCTOBA,2023". amesema Dr.Mwagike.
Sambamba na hayo Dr.Mwagike ametaja baadhi ya faida zitakazopatikana Baada ya kuanza kutumika kwa mfumo wa NeST ni pamoja na kuongezeka Kwa uwazi Kwa kuondoa Kwa kiasi kikubwa mwingiliano wa kibinadamu na maamuzi ya kibinadamu.
"Mfumo uliopo Sasa unaotoa mwanya Kwa wazabuni kumshawishi maamuzi ya vyombo husika bila vitengo vya manunuzi,Bodi za Zabuni na maafisa Masuhuli,Mfumo huu utapunguza uwezekano wa wazabuni kurubuni taasisi za umma ili wapitishwe kuomba kazi aidha Mfumo utaondoa ufanyaji wa maamuzi kwa kutumia busara au utaishi na badala yake uamuzi utatokana na uchakataji wa mfumo Kwa kuzingatia vigezo vya zabuni husika". amesema Dr.Mwagike.
Dr.Mwagike amesema Katika kuhakikisha na kuongeza ufanisi wa Mfumo huu,Mfumo wa NeST umeunganishwa na takribani mifumo kumi na nne (14) ya Serikali ili kurahisisha upatikanaji wa Taarifa zinazohitajika kwa haraka na Kwa ushahidi.
"Baadhi ya mifumo uliyounganishwa ni pamoja na Mfumo wa usajili wa makampuni wa BRELA, Mfumo wa utoaji wa leseni za Biashara (TAUSI) Wa TAMISEMI, Mfumo wa Taarifa za walipa Kodi wa TRA, na Mifumo ya GePG,MUSE, PSPTB, CRB, ERB,AQRB, OSHA,TIRA, PlanRep(Ofisi ya Msajili wa Hazina), PlanRep (TAMISEMI) na HCMIS". amesema Dr.Mwagike
Kifungu 9 (1) (k) Cha sheria ya ununuzi wa umma,sura 410 kimeipa Mamlaka ya udhibiti wa ununuzi wa umma PPRA jukumu la kubaini, kujenga na kusimamia mifumo ya kielektron Kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za ununuzi wa umma nchini.