SPIKA WA BUNGE DKT TULIA AIPONGEZA TTCL KWA KUFIKISHA HUDUMA YA MAWASILIANO KATIKA KILELE CHA MLIMA KILIMANJARO.

Na Saleh Lujuo-Dodoma.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Ackson amelipongeza shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL kwa kazi nzuri inayayofanywa na shirika Hilo ya  kuboresha huduma zake kwa wananchi hususani kufikisha huduma ya Mawasiliano katika Mlima Kilimanjaro.


Dkt Tulia ametoa pongezi hizo alipotembelea Banda la TTCL katika viwanja vya Bunge leo Mei 18.2023  Jijini Dodoma ambapo panaendelea na Maonyesho yaliyoandaliwa na wizara ya Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ili kuwaonesha wabunge shughuli za Taasisi zilizopo chini ya wizara hiyo.

"niipongeze wizara ya Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kuleta Maonyesho haya hapa Bungeni ili wabunge tuweze kujionea wenyewe mambo yanayoendelea huko katika Maeneo yetu ya uwakilishi, lakini niipongeze TTCL kwa hatua hizi mnazozichukua kutuletea huduma ya Faiba Mlangoni itasaidia sana internet majumbani na Maofisini Kwa gharama nafuu zaidi" Amesema Dkt Tulia.

Aidha,Dkt Tulia amesema atajipanga kwenda kupanda Mlima wa Kilimanjaro ili kuhakikisha huduma ya Mawasiliano katika Mlima huo ambao TTCL wamefanya kazi nzuri Katika kuliheshimisha Taifa kwenye sekta ya utalii.

"nitajipanga vizuri niende kupanda Mlima wa kilimanjaro kwa sababu nitakuwa na uhakika na mawasiliano mpaka nitakapo kuwa nafika kileleni na sasa hivi patakuwa hakuna uwongo uwongo, ukifika pale maana ndiyo upige video tujue umefika ama hujafika,nawapongeza sana TTCL kwa hatua hizo na kama mmeweza kufika katika mazingira yale ambayo ni kilele cha juu zaidi duniani kwa mlima ambao umesimama peke yake ninawapongeza sana" Amesema Dkt Tulia.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu Wa shirika la mawasiliano Tanzania TTCL Mhandisi Peter Ulanga amesema huduma ya Faiba Mlangoni itasaidia kwa kiasi kikubwa matumizi ya internet majumbani na ofisini kwa gharama nafuu.


"Tunamaeneo mbalimbali ambayo tunayaonesha Leo  kuanzia kwa T-pesa na huduma zetu mbalimbali ambazo tunazitoa,huduma za data senta ambazo tuanahudumia taasisi mbalimbali za serikali na huduma ya Mkongo Wa Taifa lakini sehemu kubwa ni kwamba huduma yetu ya Faiba Mlangoni ambayo tuanataka watu wote waweze kutumia Faiba iweze kutumia gharama zao za kutumia Mabando Majumbani" Amesema Mhandisi Ulanga.

Mhandisi Ulanga ameongezea kuwa wamepeleka huduma ya Mawasiliano katika kilele Cha Mlima kilimanjaro kwa Lengo la kukuza utalii hapa nchini.

Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL limedhamiria kutoa huduma ya Faiba Mlangoni kwa gharama nafuu ili kuwarahisishia wananchi kutumia huduma hiyo.


Post a Comment

Previous Post Next Post